Pages

Thursday, August 16, 2012

PENGINE NI VEMA WAKUSAHAU

Ninatambua wapo waliokusahau
Ninaelewa wapo ambao hawatakusahau kamwe
Mara nyingine ninatamani kuwakumbusha wengine juu yako
Lakini huwa naona ni vyema pia wakakusahua ili kupoza maumivu yao
Maana hakuna namna yoyote ya kukumbuka bila kuumia
Na siamini kama ni mapenzi yako wapenzi wako waumie