Wapendwa, Jumamosi ya Novemba 20, 2010 ndio siku maadhimisho rasmi ya kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wetu yatafanyika.
Yataanza saa 3:00 Asubuhi katika ukumbi wa M1, na kufuatiwa na maonesho mbalimbali ya kumuenzi, kukiwepo na 'Presentations' kutoka kwa watu mbalimbali na Law Sociey-SAUT.
Pamoja na kuhudhuriwa na wanachuo, jamaa na marafiki, wazazi wa Edwin pia watahudhuria, wakiambatana na ndugu wengine. Wazazi pia watapata fursa ya kuelezea maisha ya Edwin kwa ufupi na mkasa mzima uliopelekea mauti yake.
Tafadhali, mjulishe na mwenzio kuhusu kumbukumbu hii muhimu ya mtu muhimu, mpendwa wa mioyo yetu.
Roho Yake Ilazwe Mahali Pema Peponi.......... AMINA.
No comments:
Post a Comment