Pages

Saturday, September 11, 2010

Leo Katika Kumfuasa Edo

Leo nitatenda kidogo
Chembe tu ya yeye alivyokuwa,
Edo's Mom
Nitatenda kwa upole na busara
Nitamtembelea rafiki,
Kama alivyopenda kuwatembelea rafikize
Nitampigia simu rafiki
Kama alivyopenda kuwajulia hali rafikize
Sitatupa taka ovyo
Kama alivyopenda kutenda
Nitajitahidi kuwa mnyofu
Kama alivyokuwa daima
Nitasoma kitabu cha maarifa
Kama alivyopenda kusoma
Wewe Je,
Utatendaje katika kumuenzi Edo?

No comments:

Post a Comment